1.Kutoshindana na waliofanikiwa.
Daima mtu ahakikishe anawafanya waliofanikiwa wajione wapo juu. Kama mtu anataka kuwashangaza basi asionyeshe ujuzi wake wote.
Kuwapa waliofanikiwa heshima yao kutamfanya mtu apate msaada na hatimaye afikie kiwango cha juu bila ya kupata tabu nyingi.
Mfano, mtu asishindane na mwajiri wake ili kuonekana anajua sana; asishindane na tajiri katika matumizi hususani mazingira ya kijamii kama baa, misiba n.k. Waliofanikiwa hutafsiri kitendo cha kushindana kama kuonyesha kiburi au maskini jeuri.
2.Kutoamini sana marafiki.
Mtu awe makini ‘anapojamiiana’ na marafiki au watu wa karibu. Watu wa karibu huwa wasaliti na huvujisha siri kwa wapinzani. Mtu aogope marafiki zaidi ya maadui, ikibidi awape nafasi wale anaohisi ni wapinzani. Ilkiwa mtu hana wapinzani, ajitahidi kuwatafuta. Mtu ajifunze jinsi ya kutumia wapinzani kimafanikio, si kuwaamini marafiki muda wote.
3.Kuficha malengo.
Mtu afiche matarajio yake au dhamira za matendo yake. Kuweka malengo hadharani huwafanya watu wenye nia mbaya kujipanga na kuvuruga malengo husika. Mtu akinge malengo yake na ikiwa yatagundulika iwe nyakati za mwisho; nyakati ambazo wapinzani hawawezi kuweka vikwazo.
4.Kutumia wasidizi.
Kufankiwa kwa mtu kunategemea mchango anaoupata kutoka kwa wale wanaomzunguka (mazingira na marafiki). Mtu atumie busara, ujuzi na maarifa ya wale anaofanya nao kazi ili kusonga mbele. Msaada haupunguzi tu nguvu, bali pia huongeza ufanisi na kuimarisha urafiki. Mtu hupata fadhila kutoka kwa wasaidizi wake, ndipo jamii husika. Hivyo, mtu awaachie watu wengine yale wanayoweza kufanya kwa ufanisi.
5.Kushinda kupitia matendo.
Ushindi mtu anaopata kupitia maneno haufai kitu! Mtu asishindane juu ya uwezo wake kwa maneno bali, aache matendo yaongee. Ushindi makini ni ule mtu anaoupata kupitia matendo yake, na si kwa wingi wa maneno. Uhalisia wa matendo huonyesha umakini wa mtu kwa jamii inayomzunguika. Mtu husifiwa kwa kadiri ya juhudi zake za hali na mali kutatua changamoto zinazomsonga, si kwa kupiga domo.
6.Kujenga utegemezi.
Ili mtu kujua umuhimu wake katika jamii anapaswa kajua kwa kiasi gani mchango wake unahitajika. Mtu ajenge mazingira ya kutegemewa; kutegemewa kuleta furaha au ustawi katika mazingira yanayomzunguka.
Ili kfanya hivyo, mtu asitoe mbinu zote alizo nazo juu ya kitu fulani. Kutegemewa humwezesha mtu ‘kuuza’ kile alichonacho kwa mafanikio yake na ya jamii yake. Hivyo, mtu ajue wakatigani wa kuficha huduma yake, wakati gani wa ktoa kidogo na wakati gani wa kutaka watu wailipie.
7. Kutenda kama mpelelezi.
Ni muhimu sana mtu kujua juu ya wapinzani wake. Mtu atumie marafiki (wapambe) ili kupata taarifa muhimu juu ya udhaifu na uwezo wa wapinzani wake. Kufanya hivyo kutamwezesha mtu kupanga mipango ya kiulinzi na ambayo haitazimika katika safari yake ya mafanikio. Kupata taarifa kunafanikishwa kwa kuuliza maswali rahisi, kuuliza kwa njia ya upole na kwa kutumia mifano. Kila wakati ni fasaha kwa upelelezi.
8. Kuwafahamu watu wa karibu.
katika mazingira yoyote yale kuna watu wa aina nyingi. Watu hutofautiana kiimani, kitabia, kimalengo, kiutendaji n.k. Watu wa karibu ndio wanaotoa au kufanikisha kotoa ushindani katika mazingira yasiyotegemewa. Watu wengi, tena wa karibu ni kama mbwa mwitu. Ili kufahamu watu wa karibu, mtu atafakari kwa kina misingi mikuu ya urafiki huku akibadilisha muonekano, kutoa changamoto kwa walengwa n.k. Pindi mtu anapofanya yote hayo atazame mwitikio ya walengwa.
9. Kuwa na dira.
Dira humwezesha mtu kufika kule anakotaka. Mtu anapaswa kuweka malengo juu ya kule anakotaka kufika baada ya muda fulani pia, changamoto azazohisi zitamkumba sambamba na suluhu sahihi. Kwa kuwa na malengo haitakuwa ngumu sana kukabiliana na vikwazo mtu awapo safarini. Watu wengi huweka malengo huku wakisahau au kupuuzia adha zinazoweza kuwakumba au zilizowakumba watu wengine waliokuwa na malengo kama yao.
10. Kujikuza.
Mtu asipokee na kukubali sifa ‘chafu’ anazopewa na jamii. Mtu anapaswa kujikuza kwa kuvaa utambulisho mpya; ambao unavuta umakini na hauiudhi jamii yake. Mtu anapaswa kutawala taswira yale, si taswira yake ktawaliwa na nguvu kutoka nje. Kujikiza kwa jitihada za mtu huleta taswira ya kudumu, na ambayo italeta uaminifu wa kweli na kukubalika katika jamii.
11. kuwa na shabaha.
Mtu anapaswa kuelekeza nguvu na jitihada kwa yale anayoamini yataleta matunda mazuri. Mtu awe makini kutunza au kutenga nguvu za ziada kwa ajili ya changamoto. Ili kutokata tamaa, mtu anapswa kuwa na wadu (watu wa karibu) wenye uwazo tofauti tafauti kama vile madaktari, wafanya biashara, waalimu, viongozi wa dini, wazee wenye busara n.k
12. Kujirudisha nyuma.
Kama mtu akiona changamoto zitamzidi siku a usoni, huku mbinu alizo nazo au mikakati yake itakuwa dhaifu ahairishe ‘pambano’. Kurudi nyuma kutampa mtu nafasi ya kujipanga kwa kukusanya nguvu na ‘kuusoma mchezo zaidi’. Mtu asikubali kuangushwa kabisa na changamoto ndipo ajiandae kuinuka. Ni vigumu sana mtu kuamka baada ya kushambuliwa na kuangamizwa na chahangamoto za kimaisha.
13. Kutojitenga.
Kujitenga na jamii au marafiki ni hatari sana! Kwani ulimwengu ni tambara bovu na uumejaa wapinzani kila kona. Inapasa mtu kujiundia ngome ya ulinzi lakini, si kwa kujitenga. Kujitenga hupunguza mawasiliano na watu na pia uwezekano wa kupata misaada ya hali na mali. Kwa mfano, kuna uwezekano mkubwa wa kukosa habari, ushauri, vitendea kazi n.k. Vitu ambavyo ni muhimu kufikia mafanikio.
14. Kuwa muangalifu katika mahusiano
Huenda ukaanza kupata mkanganyiko juu ya mahusiano ninayoyasema, hapa nagusa mahusiano ya pande zote
(A) moja ikiwa ya kwako na jamii inayokuznguka, na hasa marafiki .Nikushauri tu huna haja ya kuwa na marafiki wengi ambao hawakusaidii kusonga mbele kimawazo na maisha,ni heri uwe na wachache ambao watakusaidia na hawatakuvuta katika njia za upotevu. Nikukumbushe msemo mmoja wa kizungu
“TOGETHER YOU STAND,,BUT ALONE YOU WILL WALK” hii ikimaanisha mtasimama pamoja kwa wingi wenu lakini mwisho wa siku utatembea kwa miguu yako mwenyewe.
(B) mbili ni mahusiano ya kimapenzi ,hili sitaligusia sana kwakuwa muda mfupi ujao nitakuletea makala maalumu lakini kwa ufupi nikuambie kwamba MPENZI WAKO WA MAISHA (KAMA UNA MALENGO NAE) anapaswa awe yule ambae anaeheshimu,anathamini na kukusaidia (hata kimawazo) ili ufikie malengo yako hii ni kwa wote yaani vijana wenzangu wa kiume na kwenu dada zangu. Kama hana mchango wowote katika utimilifu wa malengo yako SAMAHANI KWA KUKUAMBIA MNAPOTEZEANA MUDA.
15 . Mwamini Mungu
Huenda ukashangaa kwa nini hii nimeiweka mwisho badala ya mwanzo. Kwa imani yako yote uliyosoma hapo juu hayatakuwa na tija kama hutadumisha mahusiano mazuri baina yako na Mungu wako hivyo katika kila ufanyalo mtangulize Mungu na hakika utaona mafanikio.
– Dickson Mulashani kwa ushirikiano wa Mtandao
Wednesday, January 27, 2016
MBINU 15 ZA UJASIRI NA KUPATA MAFANIKIO KWENYE MAISHA.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment